Wednesday, December 22, 2010

UMASKINI WA AFRIKA SIO LAANA NI MTAZAMO.

[nyerere.jpg]                                                                                         
Mpaka sasa Afrika ndilo bara ambalo linaongoza kwa kuwa na maskini wengi zaidi duniani.Umaskini uliokithiri na unaonuka upo afrika.Pamoja na jitahidi zote zinazofanyika kutokomeza umaskini ,lakini bado kazi hii imeonekana kuwa ngumu na isiotia matumaini.Jinsi siku zinavyozidi kwenda hali ndio inazidi kuwa mbaya.waafrika wenzangu , hivi umaskini ni laana kwetu au ni mtazamo tulionao?hili swali linatakiwa kujibiwa na kila mwafrika mwenye akili timamu.
Baba wa taifa mwalimu Julius nyerere katika moja ya hotuba zake aliwahi kusema kwamba,``ukitaka kumkomboa maskini mwelimishe mtoto wake``,hii ikiwa na maana kwamba nji pekee ya kuuepuka umaskini wetu ni katika elimu.lakini swali ni je mbona watoto wengi wa afrika wameelimishwa lakini hakuna ahueni ya maisha? au kwa nini hatupati mabadiliko kutokana na elimu yao wanayoipata?tatizo ninini na kipi kifanyike?
Kama mtakuwa mnakumbuka vizuri ile ziara alioifanya mheshimiwa raisi wa Tanzania nchini marekani moja ya maswali alioulizwa ni kwa nini tanzania ni maskini? kwa kujiamini alijibu kwamba hata yeye hajui.
Katika hotuba ya mwalimu,watoto wa maskini wa Afrika aliowazungumzia ni pamoja na hawa viongozi wetu wa afrika ambao wamepata bahati ya kupata elimu [formal education] ambao ndio hasa tunawategemea watoe suluhisho hasa la nini kifanyike ili kuundoa umaskini afrika, lakini cha ajabu hata wasomi na viongozi wa juu katika nchi zetu hawajui nini kifanyike ili angalau na sisi tuweze kupiga hatua.
Au tukubaliane na msemo wa kwamba ngozi nyeusi imelaaniwa?
Ukweli ni kwamba Afrika hatujalaaniwa na wala hatujashindwa kujikwamua dhidi ya umaskini ila tatizo letu kubwa na lazima sisi waafrika tulikubali ni kwamba hatujajitambua.
Labda kabla sijaendelea mbele niwape sifa za mwanadamu ambae hajajitambua
Hawezi kujitawala mwenyewe
Hawezi kuyatawala mazingira yake mwenyewe
Hawezi kufanya maamuzi
Sio mbunifu na anategemea akili  ya mwingine kuweza kujipatia mahitaji yake
anategemea sana matumizi ya nguvu kuliko akili.hizo ni baadhi ya sifa za mtu ambae hajajitambua
Hivyo ili tuweze kuushinda umaskini lazima sisi waafrika tujitambue.Lazima tutambue ya kwamba ili tuweze kufanikiwa katika maisha lazima kuanzia sasa tujifunze kusimama kwa miguu yetu wenyewe.
Huwezi kupata mafanikio katika maisha kama wewe mwenyewe hujaamua kusimama na kukataa kubebwa.
Wenzetu wazungu wamefanikiwa sio kwa sababu wao wana akili sana kutshinda sisi ila tu wenyewe wamejitambua tayari,wanajua kwamba Mungu alituumba sio ili mazingira yatutawale bali tuyatawale.Lazima tufike hatua tukubali kwamba hatujaamua kutumia akili zetu na vipawa vyetu kutufanikisha na wakati wenzetu tayari wameshapiga hatua katika hilo.Wenzetu wanajua kwamba utajiri,heshima na uwezo wa mwanadamu kuyatawala mazingira yake uipo katika akili.Sisi tumetafsiri matumizi ya nguvu kama njia ya kutufanikisha na kutokana na hilo tunafanya kazi asubuhi mpaka jioni lakini hatupati mafanikio.

     Hii ndio Africa ya karne ya ishirini na moja.nani wa kulaumiwa?

No comments:

Post a Comment