Kwa mwanafunzi yeyote makini anaelewa kwamba kusoma silelemama.Ili ufanikiwe lazima shule uichukulie kama kazi.Hii ikiwa na maana kwamba kama mwajiliwa anavyopambana kuhakikisha anaongeza ufanisi kazini na wewe vivyo hivyo hakikisha unabuni mbinu zitakazo kufanya ufaulu. Kabla ya kukupa mbinu zitakazo kuwezesha kufanikiwa kimasomo hebu kwanza tujue ni mambo gani yanayo sababisha wanafunzi kufeli au kutokufanikiwa. 1.matatizo ya kisaikolojia:hii ina maana kwamba mwanafunzi anakuwa katika masomo lakini kichwani kunakuwa na mambo ambayo yanaondoa utulivu wa akili yake mfano migogoro ya familia,mapenzi,ukosefu wa pesa na mambo mengine mengi yanayoweza kuivuruga akili. 2.Kutokusoma kwa undani( no intensive reading).mpendwa hata kama ungekuwa na uwezo mkubwa kiasi gani kama hausomi kwa undani usitegemee kufaulu.
3.kutokuwa na muda wa kufanya marudio.Njia pekee ya kuweka mambo akilini kwa ajili ya matumizi ya baadae ni katika kurudia rudia, hivyo, kama haukumbushii unapofundishwa maana yake yale unayofundishwa yatakaa kwenye eneo la ubongo ambalo linatunza kumbukumbu kwa muda mfupi na hivyo yatafutika.unaporudia rudia kile unachokisoma kinahifadhiwa kwenye eneo la akili ambalo hutunza kumbukumbu kwa muda mrefu 4.kusoma kwa muda mrefu bila kupumzika.Ni mara nyingi kukuta wanafunzi wanakesha darasani eti wanasoma,huko ni kupoteza muda.Kusoma kunakofaa ni kwa masaa mawili tu zaidi ya hapo ni kupoteza muda. 5.Kutokujiamini:kutokuamini kwamba wewe unaweza ni moja ya mambo yanayo changia watu kufeli .Ni lazima uwe na imani kwamba unaweza kufanya jambo fulani na hapo ndipo litawezekana. 6.kutokuwa na ushirikiano:hata katika maisha ya kawaida lazima binadamu ajifunze kushirikiana na wenzie.Wewe sio Mungu hata uweze kila kitu.Unahitaji kuongeza kile unachokijua kutoka kwa wenzako,kumbuka, umoja ni nguvu,utengano ni udhaifu. 7.Ondoa uoga:tabia ya uoga si njema.Utakuta mwanafunzi anasoma huku kichwani mwake ana uoga wa kufeli hata kabla hajafanya mitihani na jinsi mwanadamu alivyoumbwa ni kwamba ukisha ingiza hofu unapunguza utendaji kazi wa akili. 8.Matumizi ya madawa ya kulevya.Vijana,hasa wa kiume hupenda wakati mwingine kuvuta sigara,bangi na vileo,hivi vyote ni sumu na vinaharibu utendaji kazi wa mwili na akili na mwisho wake ni kushindwa kufanya mambo mengine hasa ya kitaaluma 9.Imani potofu:kuamini kwamba Mungu au nguvu za giza zinaweza kukufanya ufaulu bila kusoma .ukweli ni kwamba haiwezekani kufaulu bila kusoma. 10.Kutokuwa na mpangilio mzuri wa mambo na ratiba yako.Ili ufanikiwe lazima uwe na mpangilio unaoeleweka katika kila unachokifanya.Kutokupangilia mambo yako vizuri maana yake hjui unatakiwa ufanye nini na kwa wakati gani.Huwezi kufaulu kama hauna mpangilio wa mambo yako.Lazima upange kabla ya kufanya chochote. 11.Kuwa na mtazamo hasi .Hii ikiwa ni pamoja na kuamini kwamba somo fulani ni gumu au kuamini kwamba masomo fulani ni ya watu au jinsia fulani.Huwezi kufaulu kama unawaza hasi. Mambo haya kumi ndio yanayo pelekea wanafunzi kufeli,hivyo ili mtu ufanikiwe katika masomo yako lazima ufanye yafuatayo 1.kuwa na mtazamo chanya .Mtazamo chanya ndio chanzo cha mafanikio yoyote yale,hivyo, kabla hujafanya chochote,waza chanya kwamba utaweza. 2.Soma kwa undani (intensive reading).Usiwe na papara katika kusoma.Tuliza akili ,soma mstari kwa mstari na uelewe. 3.Pata muda wa kupumzika .usisome kukesha kama nilivyo sema huku nikujichosha na kupoteza muda 4.Andaa ratiba.usisome bila ratiba .Andaa ratiba inayoeleweka.Ratiba ndio itakayokuwezesha kujua ninini usome na kwa wakati gani. 5.Vunja mada unayotaka kusoma katika vipengele vidogo vidogo vidogo ,hii itakusaidia kusoma kwa urahisi. 6.Pitia mitihani iliyopita au tunga maswali kutoka katika mada uliyosoma na uyafanye .Hii ni kujipima kama umeelewa na pia inasaidia katika kukumbushia. 7.Panua maarifa:kwa kusoma vitabu mbalimbali vinavyohusiana na mada unazozisoma darasani ,usitegemee notisi za mwalimu tu 8. Ifanye shule kama kazi.soma ukiwa na wazo kwamba elimu ndio kula yako.
No comments:
Post a Comment